08 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kinaambapo wiki ya unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama duniani, imehitimishwa Agosti 7, au jana Jumatatu, wiki iliyosheheni matukio ya kuonesha hatua za kuhakikisha watoto wanapozaliwa wananyonyeshwa maziwa ya mama kwa faida sio tu ya mtoto bali pia mama. Nchini Kenya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na Wizara ya Afya, walikuwa na tukio la aina hiyo na shuhuda wetu alikuwa mwandishi wetu nchini Kenya.