FGM

6 Februari 2019

Wanawake milioni 200 wamekeketwa, chukua hatua sasa kutokomeza FGM:UN, Mangariba  nchini Tanzania wadondosha nyembe na wakumbatia uhamasishaji dhidi ya ukeketaji na 

Sauti -
13'12"

Chukua hatua sasa kutokomeza FGM ifikapo 2030:UN

Wakati wa kuchukua hatua ili kutokomeza ukeketaji  au FGM, ifikapo mwaka 2030 ni sasa . Wito huo wa pamoja umetolewa leo ikiadhimishwa siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji na wakuu  wa mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la idadi ya watu UNFPA, Dkt. Natalia Kanem, lakuhudumia watoto UNICEF, Henrietta Fore na la linaloshughulika na masuala ya wanawake UN Women , Phumzile Mlambo-Ngcuka.

Baba alipofariki dunia ndipo FGM ikawa tishiokwetu:Msichana Elizabeth

Ukeketaji ni mila potufu ambayo inapigwa vita kote duniani hivi sasa na Umoja wa Mataifa, mashirika ya kutetetea haki za wanawake na wasicha na hata asasi za kiraia. Na wasichana walionusurika visu vya ngariba wmekuwa chachu katika vita hivi . Miongoni mwao ni binti kuitoka Tanzania.

Sauti -
1'37"

05 Februari 2019

Jaridani hii leo tumeanzia mkoani Mara nchini Tanzania ambako kituo cha Masanga kilicho kimbilio kwa watoto wa kike wanaokwepa ukeketaji sasa kimezaa matunda na wasichana ni mashuhuda.

Sauti -
11'22"

WHO  yachapisha mwongozo wa tiba dhidi ya madhara yatokanayo na FGM

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limechapisha mwongozo wa kutibu wanawake na wasichana waliokumbwa na ukeketaji, FGM.

Baba alipofariki dunia ndipo FGM ikawa tishio kwetu, Masanga iliniokoa- Msichana Elizabeth

Kuelekea siku ya kimataifa hapo kesho ya kutokomeza ukeketaji wa watoto wa kike na wasichana duniani, FGM, nchini Tanzania, kituo ambacho ni kimbilio kwa watoto wanaokwepa mila hiyo potofu, kimeendelea kuwaepusha watoto wa kike na wao sasa ni mashuhuda. 

Amchoropoka ngariba na sasa apaza sauti kupinga FGM

Harakati za kuondokana na ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake , FGM, zinazaa matunda pale msichana anapopaza sauti na jamii yake kuitikia.

Hiyo imekuwa dhahiri kwa Purity Soinato Oiyie, msichana wa kimasai kutoka Kenya ambaye akiwa na umri wa miaka 11 alikwepa kitendo hicho haramu.

Sauti -
1'19"

Polisi wanapomwepusha msichana na FGM

Ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake unasalia kuwa ni jambo linalotishia tu siyo afya ya kundi hili bali pia maendeleo yao ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Sasa watoto wenyewe wa kike wanasimama kidete kuhakikisha hawakumbwi na kikwazo hicho.

Wanaume hawana hofu tena kuoa wasichana wasiokeketwa- UNFPA

Ali Haji Hamad, Afisa Jinsia wa UNFPA Tanzania anaangazia; 

Hali ya ukeketaji nchini Tanzania hivi sasa iko vipi?

Sauti -
6'15"

Mangariba wadondosha nyembe zao Tanzania, wanaume nao wafungua masikio

Nchini Tanzania harakati za shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA zimesaidia kuepusha wanawake na watoto wa kike siyo tu dhidi ya mila hatarishi ya ukeketaji au FGM, bali pia zimesaidia kubadili mtazamo wa wanaume kuhusu kuoa wanawake ambao hawajakeketwa. Ali Haji Hamad, afisa wa jinsia kwenye ofisi hiyo amezungumza na Assumpta Massoi kwa idhaa hii.