FARC

Akiwa Colombia, Guterres ajionea maendeleo na changamoto za mkataba wa amani 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko ziarani nchini Colombia, amejionea maendeleo na changamoto za mkataba wa amani uliofikiwa nchini humo miaka mitano iliyopita kati ya serikali na wapiganaji wa zamani wa kikundi cha FARC.

Mchakato wa amani Colombia unahitaji kuungwa mkono- Massieu

Miaka miwili baada ya kutia saini makubaliano ya amani nchini Colombia na kisha kufuatia ongezeko la ghasia nchini humo, wananchi wamezindua mikakati ya kufikia maridhiano ya ujumla.

Mchakato wa amani nchini Colombia waanza kuzaa matunda: Arnault

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa ujumbe wa Umoja huo nchini Colombia, Jean Arnault amewasilisha ripoti kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo kuhusu mchakato wa amani kati ya serikali ya Colombia na waliokuwa waasi wa kundi la FARC nchini humo.

Serikali na upinzani wanaposhikamana hakuna linaloharibika

Azma ya serikali ya Colombia na kikundi cha FARC ya kuhakikisha wanatekeleza makubaliano ya amani, imekuwa ni chachu ya mafanikio yaliyopatikana hadi sasa.