Burundi sasa ni shwari tuungeni mkono katika uchaguzi:Nibigira
Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Ezechiel Nibigira ameiambia Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kuwa anakusudia baadaye hii leo kuuleza mjadala mkuu wa mkutano wa 74 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA74 pamoja na mambo mengine, kuhusu hatua za maendeleo ambazo Burundi imepiga na pia kuiomba jumuiya ya kimataifa kuiunga mkono nchi yake.