EU

Ushirikiano kati ya FAO na EU kuendelea ili kunusuru jamii hususan dhidi ya njaa

Shirika la chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO na Muungano wa Ulaya, EU, leo wamesisitiza kuendeleza ushirikiano kati yao kwa lengo la kushughulikia masuala kama vile kuongezeka kwa njaa na kuleta ustawi na amani sambamab na kujenga jamii endelevu duniani.

Hakuna mwanamke anayestahili kuuawa kwasababu ya jinsia yake:UN-EU

Umoja wa Mataifa na Muungano wa Ulaya EU leo wamezindua mkakati wa kukomesha mauaji dhidi ya wanawake na wasicha katika nchi tano za Amerika ya Kuisni kwa sababu tu ya jinsia yao, mkakati ujulikanao kama Spotlight.

Ahsante EU kwa msaada wako kwa watu wa Gaza- WFP

Muungano wa Ulaya EU umelipatia shirika la mpango wa chakula duniani, WFP zaidi ya dola milioni 3 kwa ajili ya kusaidia kununua chakula cha wapalestina walioko ukanda wa Gaza  huko Mashariki ya Kati.

Ujumuishaji wakimbizi Ureno waleta nuru mashambani

Mradi wa mfano wa kuvutia  uwekezaji na nguvu kazi nchini Ureno hivi sasa unajumuisha wakimbizi wanaowasili nchini humo kupitia mpango wa Muungano wa Ulaya wa kuwapatia makazi mapya wakimbizi.

Sauti -
2'15"

Ujumuishaji wakimbizi Ureno waleta nuru mashambani

Mradi wa mfano wa kuvutia  uwekezaji na nguvu kazi nchini Ureno hivi sasa unajumuisha wakimbizi wanaowasili nchini humo kupitia mpango wa Muungano wa Ulaya wa kuwapatia makazi mapya wakimbizi.

Jukwaa kuhusu Somalia litatawaliwa na masuala ya kiusalama, kiuchumi na kisiasa

Jukwaa la ushirika na Somalia  limeanza jumatatu mjini  Brussels Ubelgiji kujadili mambo matatu muhimu ambayo ni siasa, uchumi na usalama.Katika jukwaa hilo la, siku tatu, serikali ya Somalia pamoja na washirika wake wanaangazia njia zitakazosaidia kudumisha amani na maendeleo katika taifa hilo l

Sauti -
1'44"

Masuala ya siasa, uchumi , na usalama kutamalaki juwaa la ubia na Somalia

Jukwaa la ushirika na Somalia  limeanza leo mjini  Brussels Ubelgiji kujadili mambo matatu muhimu ambayo ni siasa, uchumi na usalama.

Mradi wa FAO na EU ‘kupiga jeki’ familia zilizoko hatarini Iraq

Jamii zilizoko hatarini katika maeneo yaliyokuwa na vita katika eneo la bonde la Ninewa magharibi mwa Mosul nchini Iraq zitaweza kuwa namnepo, kufuatia mradi wa Euro milioni 6 uliofadhiliwa na shirika la chakula na kilimo duniani, FAO na Muungano wa Ulaya, EU.

Mikakati yoyote kwa wahamiaji Ulaya izingatie haki za watoto- UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesihi Muungano wa Ulaya, EU,  na wanachama wake kuchukua hatua thabiti, za pamoja na za wakati il kuokoa Maisha ya watoto wakimbizi na wahamiaji kabla hawajaingia barani Ulaya.

IOM yapongeza Hispania kwa kukubali kuchukua wahamiaji waliokwama Mediteranea

Hatimaye Hispania imekubali kuchukua zaidi ya wahamiaji 600 waliomo kwenye boti ya Aquarius iliyowaokoa kutoka boti hatarishi baharini Mediteranea.