Tusipolinda bayoanuai tunajiangamiza wenyewe:CBD
Tatizo la kutoweka kwa bayoanuai ambayo ni muhimili mkuu wa maisha ya dunia na viumbe vilivyomo linaongezeka kila uchao na mlaumiwa mkubwa ni binadamu na shughuli zake za kila siku. Mwishoni mwa wiki Dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya bayoanuai iliyobeba kaulimbiu “sisi ni sehemu ya suluhu” Umoja wa Mataifa umetoa rai kwa kila mtu kuwajibika kuilinda bayoanuai ambayo hakuna atakayesalimika bila hiyo .