Watu zaidi ya millioni moja , wakiwemo watoto 800,000 wamesambaratishwa na ghasia za kikabila pamoja na mapigano kati ya vikosi vya serikali,dhidi ya makundi yenye silaha na makundi ya wanamgambo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo yaani DRC.