Kwingineko, Mzozo wa Syria bado unaendelea ukiingia mwaka wa tatu .Mgogoro huu umechukua sura mpya baada ya kuibuka kwa makundi ya dola la uislamu wenye msimamo mkali ISIL kundi ambalo pia linachukua kasi pia nchini Iraq.
Mwaka wa 2014 mlipuko mkubwa zaidi kuwahi kutokea wa Ebola ulizuka huko Afrika Magharibi huku ukiwauwa zaidi ya watu 7500 huku visa 19 497 vikiripotiwa na kuathiri maisha ya maelfu ya watu.
Kufahamu zaidi kuhusu migogoro Afrika na maajliwa ya bara hilo kwa mwaka ujao Jarida hili maaluam limezungumza na mwanadiplomasia na katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Afrika AU Dk Salim Ahmed Salim ambaye pia anazungumzia pia kuondolewa kwa vikwazo na uhasama kati ya Marekani na Cuba