Economic development

WFP inayashukuru mataifa kwa kusaidia kuhudumia chakula wenye njaa katika 2009

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) leo limetoa taarifa maalumu, ya shukurani, kwa Mataifa Wanachama katika sehemu zote za dunia, kwa kazi ngumu na misaada waliochangisha katika zile huduma za kupiga vita njaa ulimwenguni mnamo 2009.

UNEP itaisaidia Yemen kitaaluma, kwa kupitia mtandao, kudhibiti mazingira nchini

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) limetangaza kuwa litaipatia Yemen fursa ya kupokea makala muhimu za kisayansi, kwa kutumia taratibu za mtandao, ikiwa miongoni mwa miradi ya kujiendeleza na maarifa ya sayansi ya kisasa kwenye nchi zinazoendelea, katika kipindi ambacho mataifa haya huwa yanakabiliwa na matatizo kadha wa kadha, yanayozushwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Baraza Kuu lafanikiwa kupitisha bajeti la 2010-2011 kwa shughuli za UM

Alkhamisi iliopita, Baraza Kuu la UM lilifanikiwa kupitisha bajeti la UM kwa miaka miwili ijayo, miaka ya 2010-2011, bajeti ambalo linagharamiwa dola bilioni 5.16.

FAO imeripoti 'bei ya chai kwenye soko la kimataifa imevunja rikodi'

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limechapisha ripoti mpya yenye kuonyesha bei za chai duniani zimefikia kiwango kilichovunja rikodi, kwa mwaka huu.

Baraza Kuu laitisha Mkutano Mkuu mwakani kuharakisha utekelezaji wa MDGs

Baraza Kuu la UM limepitisha azimio la kuitisha, katika mwezi Septemba mwakani, mkutano mkuu, utakaohudhuriwa na wawakilishi wote wa kimataifa, kwa madhumuni ya kusailia maendeleo kwenye utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

Kuwasili kwa KM Copenhagen kunatazamiwa kuhamasisha mataifa kukamilisha mapatano ya COP15

Ilivyokuwa majadiliano ya Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa yanaonekana kupwelewa, na yamezorota kwenye mabishano ya kiutaratibu, pamoja na mivutano na mgawanyo mkubwa wa kimasilahi baina ya nchi tajiri na mataifa maskini,

Wataalamu wakusanyishwa Geneva na UNCTAD kuzingatia ushirikiano wa mataifa ya Kusini kuhudumia maendeleo

Shirika la UM juu ya Maendeleo na Biashara (UNCTAD) linalosimamia ukuzaji wa biashara miongoni mwa nchi zinazoendelea, ili kupiga vita ufukara na hali duni, limeanzisha mjini Geneva mkutano wa siku tatu, wenye makusudio ya kutafuta taratibu zinazofaa kuimarisha ushirikiano

Waziri Mkuu wa Kenya anazungumzia maendeleo ya uchumi kijani nchini usiochafua mazingira

Wiki hii, mjini Vienna, Shirika la UM juu ya Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) lilifanyisha kikao maalumu kuzingatia uwezekano wa Kufufua Uchumi wa Dunia kwa kutumia Viwanda Kijani, yaani viwanda vitakavyotunza mazingira.

Ripoti ya FAO yanonyesha bei za chakula zimeanza kupanda tena kwenye soko la kimataifa

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limehadharisha kwenye ripoti iliochapishwa Ijumatano kwamba bei za juu za chakula, zimeanza kupanda tena katika dunia.

Bidhaa za ndizi, kwenye soko la kimataifa, hazijaathirika na migogoro ya uchumi, imeripoti FAO

Mazao ya ndizi ni bidhaa ya kilimo inayotarajiwa kutoathirika na mizozo ya kifedha, iliotanda karibuni kwenye soko la kimataifa, kwa mujibu wa ripoti iliochapishwa mapema wiki hii na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO).