Economic development

Mkutano wa Doha Kugharamia Maendeleo kuthibitisha tena Mwafaka wa Monterrey

Maofisa wa ngazi za juu kutoka zaidi ya nchi 160, ikijumlisha Viongozi 40 wa Taifa na Serikali walikusanyika kwenye mji wa Doha, Qatar - kuanzia tarehe 29 Novemba hadi 02 Disemba 2008 - kufanya mapitio na tathmini ya pamoja kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya Muafaka wa Monterrey, Mexico ya 2002 yaliokusudiwa, hasa, kuharakisha shughuli za kuimarisha uchumi maendeleo kwa jamii za nxchi maskini.

Matokeo ya Mkutano wa Doha yamvunja moyo Mtaalamu wa Haki za Binadamu

Dktr Cephas Lumina, Mkariri Mtaalamu Huru wa UM anayezingatia masuala ya haki za binadamu na athari za madeni, ametoa taarifa ilioangaza matoeko ya Mkutano Mkuu wa Kimataifa juu ya Ugharamiaji wa Misaada ya Maendeleo, uliomalizika mwanzo wa wiki kwenye mji wa Doha, Qatar.

Mkutano wa kugharamia maendeleo wakaribia hatima

Mkutano wa Kimataifa juu ya Ugharamiaji wa Maendeleo unaofanyika kwenye mji wa Doha, Qatar leo umeingia siku ya tatu na unakaribia kuhitimishwa. Kikao kinafanya mapitio ya mapendekezo yaliopitishwa 2002 kwenye mkutano wa Monterrey, Mexico; mapatano yalioafikiana kuwepo ushirikiano mkubwa baina ya nchi zenye maendeleo ya viwanda na nchi maskini kugharamia misaada ya maendeleo, hasa katika kuandaa misaada rasmi ya kigeni, masharti ya kibiashara yanayoridhisha na kusamehe madeni ya nchi zinazoendelea. KM kwenye risala yake alitilia mkazo umuhimu wa “kuhakikisha watoto wote huwa wanafadhiliwa ilimu ya msingi, ilimu ambayo ikikosekana nchi husika zinazoendelea zitashindwa kukamilisha malengo yao ya maendeleo.” Alisema watoto milioni 75 duniani, hivi sasa, wamenyiwa fursa ya kupata ilimu, na mamilioni ziada katika mataifa masikini hupatiwa ilimu, lakini ya kiwango cha chini kabisa kuwawezesha wao kujihudumia kimaisha.

Siku ya Kuhamasisha Maendeleo ya Viwandani Afrika

UM unaadhimisha Siku ya Kukuza Maendeleo ya Viwanda Afrika. Risala ya KM kuihishimu siku hii ilitilia mkazo ya kuwa shughuli za kukuza viwanda katika Afrika ikitekelezwa itaashiria hatua itakayosaidia pakubwa kudhibiti, kwa mafanikio, matatizo ya chakula, fedha na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na, hatimaye, kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na jamii ili kuufyeka umaskini katika bara hilo.

Mkutano wa kimataifa Cambodia wajadilia nidhamu za kuzisaidia nchi maskini sana kibiashara

Mawaziri wa biashara na viwanda kutoka nchi masikini za kiwango cha chini kabisa duniani, wanakutana hii leo kwenye mji wa Siem Reap, Cambodia katika mkutano wa siku mbili kuzingatia taratibu za kufungamanisha uchumi wao na mfumo wa biashara [uliopo] katika soko la dunia.

UNCTAD inahimiza nchi masikini zifadhiliwe misaada ya kiuchumi kujikinga na matatizo ya fedha

Kwenye kikao cha 45 cha Bodi la Utendaji la Shirika la UM juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD) kilichofanyika Geneva Ijumaa ya leo, KM wa taasisi hiyo, Supachai Panitchpakdi alikumbusha ya kuwa wakati umewadia kwa Mataifa Wanachama wa UM, kushirikiana kidharura, kubuni mfumo wa marekibisho kukabiliana na mgogoro wa fedha kwenye soko la kimataifa.

Wachumi wa Afrika wanakutana Tunis kusailia sera zifaazo kuimarisha maendeleo

Wataalamu wa uchumi pamoja na wabunisera wa kutoka nchi kadha za Afrika wamekutana hii leo kwenye mji wa Tunis, Tunisia kuanza mkutano wa siku tatu kushindiliza utekelezaji imara wa miradi ya uchumi kwenye nchi zao.

UN-HABITAT inazingatia hali ya miji duniani kwa 2008/09

Shirika la UM juu ya Makazi (UN-HABITAT) limewasilisha ripoti mpya juu ya Hali ya Utulivu wa Miji Duniani kwa 2008/2009.

Mtaalamu juu ya Makazi anasema 'mfumo wa soko huru pekee hauwezi kusuluhisha matatizo ya mikopo ya nyumba'

Mkariri Maalumu wa UM juu ya Makazi Bora, Raquel Rolnik alasiri anatarajiwa kuzungumzia Baraza Kuu juu ya athari za matatizo ya mikopo ya nyumba iliozuka, hasa katika mataifa yalitoendelea katika miezi ya karibuni.

Raisi wa BK ameanzisha tume maalumu ya kupitia mfumo wa fedha duniani

Raisi wa kikao cha 63 cha Baraza Kuu la UM, Miguel d’Escoto ametangaza kuanzisha tume maalumu ya hadhi ya juu kabisa, itakayofanya mapitio juu ya mfumo wa fedha wa kimataifa kama unahitajia marekibisho, ikijumlisha pia zile taasisi za fedha za kimataifa kama Benki Kuu ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).