Economic development

Mataifa ya KiAfrika na FAO yaahidi kuimarisha elimu vijijini

Mataifa 11 ya KiAfrika, yalikutana karibuni mjini Rome, Utaliana kwenye Makao Makuu ya Shirika la UM la Chakula na Kilimo (FAO) na yaliafikiana kushiriki kwenye ule mradi wa kuimarisha elimu ya msingi vijijini, kwa dhamira ya kusaidia wakazi wa maeneo hayo kujipatia ujuzi wa kupiga vita, kwa mafanikio, ufukara, matatizo ya njaa, utapia mlo na kutojua kusoma na kuandika. Maafa haya ya kijamii huathiri zaidi mataifa ya Afrika yaliopo kusini ya Sahara.

Afrika itayari kupokea vitegauchumi kuimarisha teknolojia ya mawasiliano ya kisasa

Mkutano Mkuu wa Kuunganisha Afrika kwa kutumia njia ya teknolojia ya mawasiliano ya habari ya kisasa ya kompyuta, ulifanyika wiki hii kwa siku mbili mjini Kigali, Rwanda kwa lengo la kuboresha na kuimarisha maendeleo barani humo.

Hapa na pale

UM, ikishirikiana na makampuni ya kimataifa ya Googles na Cisco, yenye kuongoza katika taaluma na teknolojia za ,awasiliano ya kisasa yameanzisha kipamoja anuani mpya ya mtandao itakayompatia mtumiaji kompyuta fursa ya kufuatilia, kihakika, namna miradi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) inavyotekelezwa na kuendelezwa katika maeneo mbalimbali ya dunia. ~

Utekelezaji wa MDG katika sekta afya mkoani Tabora, Tanzania (Sehemu ya Pili)

Katika makala iliopita tuliripoti kwamba karibuni nilipata fursa ya kutembelea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nilipokuwa huko nilizuru moja ya vijiji kumi vilivyochaguliwa rasmi na UM barani Afrika kuwa vjiji vya milenia.

Juhudi za kukamilisha MDGs Tabora, Tanzania

Hivi karibuni nilizuru Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nilipatiwa fursa ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliohusishwa kwenye huduma za utekelezaji wa ile miradi ya UM ya inayoambatana na Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

Mawaziri wanazingatia msukumo mpya kugharamia maendeleo

Mkutano wa Hadhi ya Juu ulifanyika kwenye Makao Makuu mjini New York kusailia hatua za kuchukuliwa kukamilisha maafikiano yaliopitishwa mwaka 2000 kwenye mji wa Monterrey, Mexico. Maafikiano ya Monterrey hasa yalidhamiria kuongeza ushirikiano wa kiuchumi wenye nguvu, na ulio bora, kwa umma wa kimataifa ili kupiga vita umasikini. Maafikiano ya Monterrey yalipendekeza kuzingatiwe masuala yanayoambatana na usimamizi wa kizalendo wa gharama za kuhudumia maendeleo; na kusailia taratibu madhubuti za ugawaji wa misaada ya kimataifa. ~~Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.

Mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro alifanya mazungumzo maalumu na Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM ambapo alichukua fursa hiyo kufafanua mwelekeo mpya kuhusu kazi na shughuli za UM duniani. Alisailia juu ya juhudi za KM Ban Ki-moon katika kuharakisha utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs), kwa wakati, Afrika kusini ya Sahara. Kwenye makala hii ya awali ya mahojiano yetu Naibu KM Migiro anazugumzia mada mbili: awali, utekelezaji wa Malengo ya MDGs Afrika kusini ya Sahara na, pili, suala la Darfur. ~~Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.

Hapa na pale

Ofisi ya UM juu ya Udhibiti wa Uhalifu na Madawa ya Kulevya Ulimwenguni (UNDOC), ikijumuika na Benki Kuu ya Dunia, wameanzisha Taratibu za kisheria Kuhakikisha Mali za Umma Zilioibiwa Zinafidiwa, kitendo kilichokusudiwa kuyasaidia mataifa masikini kurejeshewa rasilmali ya taifa iliyoibiwa na viongozi walaji rushwa, ambao walizipatia akiba hizo hifadhi kwenye vyombo vya fedha vya kigeni; fedha hizi zitakapopatikana zinatarajiwa kutumiwa kuendeleza huduma za kiuchumi na jamii zenya natija kwa taifa zima.~

Mkutano wa viongozi kuimarisha uwezo wa utekelezaji wa nchi za Kiafrika

Akifungua mkutano wa pili wa viongozi ulotayarishwa na taasisi ya kuimarisha uwezo wa utekelezaji barani Afrika, ACBF mjini Maputo Msumbiji, Rais Armando Guebuza wa Msumbiji, alisema suluhisho kwa matatizo ya Afrika yanabidi kutanzuliwa kwa kuendelea kuimarisha uwezo wa taasisi zake, kwa upande wa watumishi, fedha na mali.

WFP inahitajia dola milioni 22.4 kukidhia mahitaji ya chakula kwa Wasomali

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeomba lifadhiliwe na jamii ya kimataifa mchango wa dola milioni 22.4 kukidhia mahitaji ya chakula kwa Wasomali milioni 1.2 katika jimbo la Shabelle, Usomali.