Wanasayansi wa bahari na mashirika yasiyo ya serikali wataka hatua za kulinda bahari
Ripoti maalum ya Jopo la kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, IPCCC ikiangazia hali ya bahari na sehemu zenye theluji imefichua kiwango cha janga linalowakodolea binadamu wakati bahari zinaanza kuonesha dalili za kuporomoka.