DRC

Mashirika ya UN yaendelea kufikisha nuru kwa wakimbizi huko Ituri DRC 

Katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake umeendelea kusambaza misaada kwa wakimbizi wa ndani ambao walilazimika kukimbia makwao na kuacha kila kitu na hivi sasa wanaishi kwenye kambi za wakimbizi hususan katika eneo la Pinga jimboni humo. Misaada hiyo imekuwa jawabu kwa wakimbizi ugenini.

ADF yakatili maisha ya mamia ya watu na kutawanya wengine 40,000 DRC:UNHCR 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UHNCR limetoa onyo kuhusu kuongezeka kwa idadi ya mashambulizi yanayofanywa na makundi yaliyojihami dhidi ya raia kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.  

12 Machi 2021

Hii leo jaridani Ijumaa ya tarehe 12 machi 2021 Flora Nducha anakuletea mada kwa kina ikibisha hodi huko Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kukutana na familia ambayo inamletea mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minane baada ya kumuokoa msituni wakati wa mashambulizi kutoka kwa waasi

Sauti -
11'55"

"Nilisikia sauti usiniache! ndipo nikakuta mtoto Anuarita"- Asema baba aliyenusuru mtoto msituni huko DRC

Anwarita mtoto mwenye  umri wa miaka 8 amejikuta yatima baada ya waasi kuua kwa mapanga wazazi wake huko Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Hivi sasa Anwarita anaishi na familia iliyomnusuru msituni, wakati huu ambapo takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasema kwa sasa watoto milioni 3 nchini humo wametawanyishwa na mizozo.
 

UNHCR yafanya juhudi za kuwaokoa wanaoikimbia CAR kuingia DRC.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linafanya kazi ya kuwahamisha maelfu ya wakimbizi wa Afrika ya Kati wanaoishi katika makazi ya muda mpakani mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwenda kwenye maeneo salama ambapo wanaweza kupata msaada wa kibinadamu na ulinzi.

26 Februari 2021

Leo Ijumaa ni mada kwa kina ikijikita huko jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako walinda amani wanawake kutoka Tanzania wakihudumu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa.

Sauti -
11'11"

Askari walinda amani wanawake kutoka Tanzania wawatembelea wanawake Beni, DRC

Kikundi cha walinda amani wanawake kutoka Tanzania katika kikosi cha nane kinachohudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa FIB MONUSCO, nchini DRC, kimewatembelea wanawake wa kata za Matembo, Nzuma na Ngadi wilaya ya Beni. 

Jamii ya kimataifa ikihaha kunusuru DRC, jamii yashikamana kupunguza madhila

Ikiwa leo ofisi ya Umoja wa MAtaifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA inapatia nchi wanachama wa Umoja huo hali halisi ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, , raia nchini humo licha ya machungu wanayopitia na madhila yanayowakabili  wameendelea kuonesha mshikamano wa a

Sauti -
2'32"

24 Februari 2021

Hii leo jaridani tunaanzia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako wananchi licha ya madhilla wanayopitia mashariki mwa nchi hiyo wanashikamana na wanasaidiana ili angalau kupunguza machungu.

Sauti -