DRC

Zaidi ya watoto 170 wanahofiwa kupotea kufuatia mlipuko wa volkano Goma, DRC 

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, leo Jumapili limesema kwamba mamia ya watoto na familia katika mjini Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC wako katika hatari kufuatia mlipuko wa volkano wa Mlima Nyiragongo. 

Naishukuru FAO na WFP mimi na wanangu 12 twaweza kuishi: Mjasiriamali Furaha 

Mradi unaoendeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP na la chakula na kilimo FAO wa kuongeza usawa wa kijinsia na mahusiano mema kwenye jamii umekuwa mkombozi wa wanawake wengi kwenye eneo la Kasheke Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, akiwemo Furaha Josee ambaye ni mama mjasiriamali mchuuzi wa sokoni.

Tunalaani vikali shambulio dhidi ya MONUSCO Kivu Kaskazini:UN 

Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulio lililofanyika jana Jumatatu dhidi ya eneo la muda la mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC katika mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini. 

Mlipuko wa 12 wa Ebola Kivu Kaskazini umetokomezwa - WHO 

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO hii leo kupitia taarifa iliyotolewa mjini Brazzaville Congo na  Kinshasa, DRC, limetangaza kumalizika kwa mlipuko wa 12 wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, miezi mitatu tu baada ya mgonjwa wa kwanza kuripotiwa Kivu Kaskazini.  

UNAOC imelaani vikali mauaji ya mwakilishi jumuiya ya Kiislamu Beni DRC 

Mwakilishi wa ngazi ya juu Muungano wa Ustaarabu wa Umoja wa Mataifa (UNAOC), Bwana Miguel Ángel Moratinos, amelaani vikali mauaji ya kinyama ya mwakilishi wa jumuiya ya Kiislamu yaliyofanyika katika mji wa Beni mashariki mwa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakati wa swala ya jioni katika msikiti wa kati.  

Je unawezaje kuanza upya maisha ukiwa umepoteza kila kitu:Mkimbizi Fidel

Kutana na mkimbizi Fidel kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ambaye hivi sasa anaishi kwenye kambi ya wakimbizi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Fidel alipoteza kila kitu ikiwa ni pamoja na mwanaye wa kiume machafuko yaliposhika kasi CAR na ikamlazimu kufungasha virago na kukimbia, sasa anajaribu kujenga upya maisha yake ukimbizini.

Mtu mmoja kati ya 3 DRC anakabiliwa na njaa kali, wengi wategemea mzizi Taro 

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hali ya ukosefu wa chakula inazidi kuwa mbaya ambapo mtu mmoja kati ya watu watatu anakabiliwa na njaa kali, yamesema hii leo mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la chakula na kilimo, FAO na lile la mpango wa chakula duniani, WFP.  

 

Gbagbo na Blé Goudé huru, Ntaganda ang’ang’aniwa

Mahakama ya rufaa ya mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC leo imetupilia mbali rufaa ya mwendesha mashtaka wa ICC dhidi ya uamuzi wa mahakama hiyo ya kuwaachi huru rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo na aliyekuwa mkuu wa vijana Charles Blé Goudé.
 

Nchini DRC mashirika ya UN yaendelea kuwa mkombozi kwa wakimbizi

Katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake umeendelea kusambaza misaada kwa wakimbizi wa ndani ambao walilazimika kukimbia makwao na kuacha kila kitu na hivi sasa wanaishi kwenye kambi za wakimbizi hususan katika eneo la Pinga jimbo

Sauti -
2'35"

24 MACHI 2021

Katika jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Grace Kaneiya anakuletea 

- Ikiwa leo ni siku ya kifua Kikuu duniani Umoja wa Mataifa umetangaza habarin njema ya tiba ambayo sio tu gharama yake ni nafuu bali pia ni ya muda mfupi na vidonge vinavyotumika ni vichache.

Sauti -
12'37"