DRC

02 JUNI 2021

Hii leo jaridani Leah Mushi anaanzia huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako waasi wa ADF wameshambulia kambi za wakimbizi wa ndani na kuua raia 55, UN umetoa taarifa ya kulaani.

Sauti -

Volkano ya Nyiragongo imesambaratisha maisha yetu- Mkimbizi kutoka DRC 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wengine wanawasaidia watu waliolazimika kuyakimibia makazi yao baada ya mlipuko wa volkano katika Mlima Nyiragongo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC. Wengi walivuka mpaka kwenda nchi jirani ya Rwanda ambako sasa wanapata usaidizi.

UN yalaani mauaji ya raia 55 yaliyofanywa na ADF mashariki mwa DRC 

Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mashambulio ya siku ya Jumatatu yaliyofanywa na waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) dhidi ya wakimbizi wa ndani huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kusababisha vifo vya raia 55 na wengine wengi wamejeruhiwa.

Watu 350,000 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu Goma DRC:UNHCR 

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema msaada wa haraka wa kibinadamu unahitajika kuwasaidia maelfu ya watu walioathirika na mlipuko wa volcano iliyolipuka tarehe 22 Mei mwaka huu kwenye mlima Nyiragongo mjini Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. 

28 MEI 2021

Katika Jarida la mada kwa kina hii leo Leah Mushi anakuletea

Sauti -
12'21"

Hofu ya kulipuka tena volkano Nyiragongo yafurusha maelfu Goma 

Maelfu ya wakazi wa mji wa Goma ulioko jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hawana makazi hivi sasa na wako kwenye harakati za kuhama hata kule walikokimbilia karibu na mji huo bada ya mamlaka kuwaagiza wahame kwa hofu ya kwamba volkano katika Mlima Nyiragongo inaweza kulipulka tena. 

UNHCR na wadau watathmini kiwango cha mahitaji kufuatia mlipuko wa volkano Nyiragongo

Idadi ya watu waliokufa kutokana na mlipuko wa volkano katika mlima Nyiragongo jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imeongezeka na kufikia wawtu 32 huku Umoja wa Mataifa ukiongeza jitihada za kufikisha misaada. Flora Nducha na maelezo zaidi.

Sauti -
1'51"

25 Mei 2021

Hii leo jaridani tunaanzia huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumulika janga la mlipuko wa volkano katika mlima Nyiragongo jimboni Kivu Kaskazini.  Kisha tunaangazia ripoti ya

Sauti -
13'36"

UNFPA na Taasisi ya Panzi DRC yaingia makubaliano kunusuru manusura wa ukatili wa kingono 

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yamekuwa mwiba siyo tu katika usalama wa taifa hilo bali pia kwa wanawake na wasichana ambao hukumbwa na ukatili wa kingono kule kwenye mapigano. Mashirika ya kiraia yamekuwa yakiunga mkono harakati za Umoja wa Mataifa

Sauti -
4'57"

24 MEI 2021

-Katika jarida la mada kwa kina hii leo kutoka Umoja wa Mataifa Leah Mushi anakuletea 

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mlipuko wa volkano katika mlima Nyiragongo mjni Goma jimboni Kivu Kaskazini umesababisha vifo vya watu 15. 

Sauti -
11'10"