DRC

Waasi 22 wauawa huko Ituri, MONUSCO yadhibiti shambulio lao 

Takribani watu 30 wameuawa kufuatia shambulio la jumatatu huko Kinyanjojo na Boga kwenye jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. 

Takribani watu 6,000 wamekimbia makazi ya dharura kutokana na mashambulizi DRC- UNHCR 

Mashambulizi makali yanayotekelezwa na waasi wa kundi la Allied Democratic Forces ADF, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC yamewalazimisha watu 5,800 kukimbia mara kadhaa katika makazi ya watu waliotawanywa katika jimbo la Ituri Mashariki mwa nchi hiyo. 

Wanawake na wasichana wakimbizi wahaha kupata taulo za kike DRC, UNHCR yawasaidia 

Wanawake na wasichana wakimbizi waliotawanywa na machafuko nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu kupata taulo za kike kila mwezi kutokana na gharama huku wakijaribu kulinda uhai wao na kuhudumia familia zao baada ya kukimbia vita. Lakini sasa kwa msaada wa mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wanaweza kujishonea taulo hizo na kujisitiri.

Volkano ya Nyiragongo imesambaratisha maisha yetu- Mkimbizi kutoka DRC 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wengine wanawasaidia watu waliolazimika kuyakimibia makazi yao baada ya mlipuko wa volkano katika Mlima Nyiragongo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC. Wengi walivuka mpaka kwenda nchi jirani ya Rwanda ambako sasa wanapata usaidizi.

UN yalaani mauaji ya raia 55 yaliyofanywa na ADF mashariki mwa DRC 

Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mashambulio ya siku ya Jumatatu yaliyofanywa na waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) dhidi ya wakimbizi wa ndani huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kusababisha vifo vya raia 55 na wengine wengi wamejeruhiwa.

Watu 350,000 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu Goma DRC:UNHCR 

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema msaada wa haraka wa kibinadamu unahitajika kuwasaidia maelfu ya watu walioathirika na mlipuko wa volcano iliyolipuka tarehe 22 Mei mwaka huu kwenye mlima Nyiragongo mjini Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. 

Hofu ya kulipuka tena volkano Nyiragongo yafurusha maelfu Goma 

Maelfu ya wakazi wa mji wa Goma ulioko jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hawana makazi hivi sasa na wako kwenye harakati za kuhama hata kule walikokimbilia karibu na mji huo bada ya mamlaka kuwaagiza wahame kwa hofu ya kwamba volkano katika Mlima Nyiragongo inaweza kulipulka tena. 

Zaidi ya watoto 170 wanahofiwa kupotea kufuatia mlipuko wa volkano Goma, DRC 

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, leo Jumapili limesema kwamba mamia ya watoto na familia katika mjini Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC wako katika hatari kufuatia mlipuko wa volkano wa Mlima Nyiragongo. 

Naishukuru FAO na WFP mimi na wanangu 12 twaweza kuishi: Mjasiriamali Furaha 

Mradi unaoendeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP na la chakula na kilimo FAO wa kuongeza usawa wa kijinsia na mahusiano mema kwenye jamii umekuwa mkombozi wa wanawake wengi kwenye eneo la Kasheke Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, akiwemo Furaha Josee ambaye ni mama mjasiriamali mchuuzi wa sokoni.

Tunalaani vikali shambulio dhidi ya MONUSCO Kivu Kaskazini:UN 

Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulio lililofanyika jana Jumatatu dhidi ya eneo la muda la mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC katika mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini.