DRC

Watu 80,000 waathiriwa na mafuriko makubwa DRC

 Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Andrej Mahecic hii ameviambia vyombo vya habari mjini Geneva Uswisi kuwa UNHCR inashirikiana na mamlaka pamoja na wadau nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kutoa msaada kwa watu 80,000 ambao wameathiriwa na mafuriko makubwa katika jimbo la Kivu Kusini. 

Siku chache kabla ya DRC kutangaza mwisho wa Ebola, mgonjwa mpya agundulika

Siku chache kabla ya ulimwengu kutangaza kuutokomeza ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC,  Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus kupitia ukurasa wake wa twitter Ijumaa ya leo, kwa masikitiko ametangaza kubainika kwa mgonjwa mpya wa Ebola nchini humo.

Dola milioni 621 zasakwa kusaidia wakimbizi na wenyeji DRC

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wake huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wanaomba dola milioni 621 ili kusaidia raia wa taifa hilo waliosaka hifadhi nchi jirani sambamba na wale wanaowahifadhi.

Mgonjwa wa mwisho wa Ebola DRC aruhusiwa kurejea nyumbani, 46 bado wanachunguzwa

Taarifa ya shirika la afya ulimwenguni WHO iliyotolewa jana mjini Brazzaville Congo na Goma Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, imesema kuwa habari njema ni kuwa mgonjwa wa mwisho wa Ebola nchini DRC ameruhiswa kurejea nyumbani baada ya kupatiwa matibabu katika kituo cha matibabu huko kaskazini mashariki mwa mji wa Beni.

WHO imehimiza umuhimu wa serikali kudhibiti virusi vya corona.

Shirika la afya ulimwenguni, WHO leo Jumatatu limehimiza umuhimu wa serikali kuendelea kuweka kipaumblele katika kuzuia na kudhibiti virusi vya corona.

Visa vipya vinne vya Ebola vimethibitishwa DRC kati ya Januari 29 na Februari 4-WHO

Taarifa ya WHO kuhusu tathimini na mwenendo wa maambukizi ya Ebola imesema kuanzia tarehe Januari 29 hadi Februari 4, visa vinne vipya vilivyothibitishwa viliripotiwa katika milipuko unaoenea wa ugonjwa wa virusi vya Ebola (EVD) katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kamishina Mkuu haki za binadamu ahitimisha ziara DRC, atoa wito

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet hi leo tarehe 27 Januari amehitimisha ziara yake ya siku tano nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

Bachelet yupo Ituri DRC kujadili ghasia za kikabila

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amewasili Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC leo asubuhi kwa saa za huko na kuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya haki za binadamu na wajumbe wa kamati ya usalama wa jimbo hilo ambalo hivi hivi karibuni limekuwa limegubikwa na changamoto za kiusalama kutokana na mapigano ya kati ya wahema na walendu.

Mkakati wa UN na DRC wapaswa kushughulikia changamoto za usalama:Tume

Serikali nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO wametakiwa kuunda mkakati wa kina wa pamoja ili kushughulikia changamoto za usalama kwenye eneo la Beni, jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa DRC.

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kuzuru DRC wiki hii

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet Alhamisi wiki hii ataanza ziara ya siku tano nchini Jamhuri ya Kidemokarsia ya Congo, DRC kwa mwaliko maalum wa serikali.