Janga la njaa DRC linazidi kuwa baya kutokana na mapigano na ukosefu wa ufadhili wa misaada - WFP
Mgogoro katika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) unaendelea kuwa mbaya huku mapigano yakizidi, na kusababisha makumi ya maelfu ya watu kukimbia makazi yao na kuzidisha njaa kali, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeeleza leo Novemba 7.