Wakati Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania ikiwa imepata uongozi mpya kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais wa Taifa hilo la Afrika Mashariki, John Magufuli, Waziri wa Katiba na Mambo ya Sheria Dkt. Augustine Mahiga amezungumzia majukumu ya tume hiyo wakati huu ambapo tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limetimiza miaka 71 tangu kupitishwa.
Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiwa umeingia siku ya tatu hii leo, Tanzania itatumia nafasi yake ya kuhutubia hii leo, kutangaza msimamo wake na chombo hicho chenye wanachama 193.