dijitali

UN News/Patrick Newman

Lengo letu ni kuhakikisha kwamba wanawake na wasichana wanaonekana kidijitali-Sambuli

Kwa miaka mingi, wanawake walikuwa wakiachwa nyuma katika maendeleo na hata maswala ya kijamii ikichochewa na utamaduni na mitazamo dume kwenye jamii. Kwa kutambua hilo Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba tano la malengo ya maendeleo endelevu linalenga kuziba pengo hilo ambalo kwa miaka limebinya haki za wanawake na wasichana. Moja ya maeneo ambako mwanamke ameachwa nyuma ni ulimwengu wa dijitali na kwa kutambua hilo Katibu Mkuu aliunda jopo maalum kwa ajili ya kusongesha malengo hayo mbele.

Sauti
3'39"

16 JANUARI 2020

Katika Jarifada la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Watu milioni 45 katika nchi 16 za Kusini mwa Afrika maisha yao yako hatarini kutokana na njaa, na hatua za haraka za msaada zinahitajika limesema shirika la Umoja wa Matafa la mpango wa chakula duniani WFP

-Kimbunga Idai kilifungua macho ya madhila yanayowasibu watu wenye ulemavu nchini Zimbawe kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na elimu, UNESCO

Sauti
11'44"
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakifufua filamu za kihistoria zilizohifadhiwa kwenye maktaba ya kumbukumbu ya chombo hicho. (Picha hii ni ya Novemba 2004)
UN /Mark Garten

Umoja wa Mataifa waangazia kuzihifadhi sauti na picha kwa mfumo wa kidijitali ili kuhifadhi historia ya binadamu

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya urithi wa sauti na picha, Umoja wa Mataifa unatambua kazi ngumu ya maelfu ya wataalamu wa kuhifadhi nyaraka wakiwemo wakutubi na watunza nyaraka ambao maarifa yao  na kujitolea kwao vinasaidia kuhakikisha kuwa dunia haipotezi historia yake ya filamu za kale, redio na televisheni.