Majanga lukuki yasababisha ukuaji finyu wa uchumi duniani
Mchanganyiko wa majanga lukuki umechochea kiwango kidogo zaidi cha ukuaji wa uchumi duniani kuwahi kushuhudiwa katika miongo ya hivi karibuni na mwelekeo unazidi kutia shaka, imesema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo ikimulika ukuaji uchumi mwaka jana na makadirio kwa mwaka huu.