#Dataforum

OCHA/Rita Maingi

Elimu kuhusu hifadhi ya jamii Tanzania kusaidia kupanua wigo

Wakati Umoja wa Mataifa ukieleza kuwa upataji wa huduma za hifadhi ya jamii bado ni changamoto kubwa wa wakazi wengi wa dunia, Tanzania imeamua kuchukua hatua madhubuti kwa kutambua kuwa hifadhi  bora ya jamii ni jawabu la siyo tu kupunguza umaskini wa  kaya bali pia umaskini katika ngazi ya taifa.

Tanzania imechukua hatua kuhakikisha hifadhi ya jamii inakuwa na manufaa si tu kwa wafanyakazi walio kwenye sekta rasmi ambao wanachangia mifuko hiyo, bali pia kundi kubwa la watu walio kwenye sekta isiyo rasmi wakiwemo wanawake.

Sauti
1'28"
Kongamano la Umoja wa Mataifa la takwimu Duniani
Nembo na UN/World Data Forum

Wataalam wa takwimu wakutana kusaka suluhu za changamoto zinazoikabili dunia:    

Wataalam wa kimataifa wa takwimu kutoka ofisi za kitaifa, sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali yaani NGO’s, wanazuoni, na mashirika ya kimataifa na kikanda, wamekusanyika mjini Dudai katika Falme za Kiarabu kuanzia leo katka jitihada za kusongesha mbele mchakato wa kutimiza malengo ya maendeleo endelevu au SDG’s.