Syria: Dungusikakati ni mkombozi kwa wafugaji na mazingira - FAO
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO linawasaidia wakulima wanaoishi katika mazingira magumu katika viunga vya nje kidogo ya mji mkuu wa Syria, Damascus kukabiliana vyema na mabadiliko ya tabianchi kwa kulima mimea ya dungusikakati isiyo na miba ili waweze kuwalisha mifugo wao hasa nyakati za ukame. Taarifa ya Anold Kayanda inafafanua zaidi.