Pamoja na mafanikio makubwa bado kuna changamoto kumjumuisha kikamili mwanamke mwenye ulemavu Zanzibar: Ms. Abeida Abdallah
Kisiwa cha Zanzibar nchini Tanzania Mashariki mwa Afrika kimepiga hatua kubwa katika suala la ujumuishaji wa watu wenye ulemavu katika sekta mbalimbali kwa kuzingatia mikataba ya Umoja wa Mataifa ya watu wenye ulemavu na pia usawa wa kijinsia kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma. Lakini licha ya mafanikio waliyoyapata katika masuala kama elimu na haki za watu wenye ulemavu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi.