Chuja:

CRPD

UN News

Tanzania inatekeleza kwa vitendo mkataba wa haki za watu wenye ulemavu- Mbunge Amina

Leo ni siku ya watu wenye ulemavu ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa ujumbe wake akisema kuwa, “tunapolinda haki za watu wenye ulemavu, tunasonga mbele kufikia ahadi kuu ya Ajenda ya 2030 - kutowaacha yeyote nyuma,”  akisema kuwa, hata hivyo bado kuna mengi ya kufanya, tumeona maendeleo muhimu katika kujenga ulimwengu jumuishi kwa wote.

Sauti
3'15"
Hapa ni kwenye moja ya soko nchini Thailand, wadudu wakiuzwa kama kitoweo.
P.B. Durst

Miongoni mwa tulizokuwa nazo wiki hii

Watu wenye ulemavu wakumbukwe katika suala la utalii-Mbunge Tanzania. Mtu 1 kati ya 3 duniani hana fursa ya kupata maji safi ya kunywa na huduma za kujisafi- UNICEF/ WHO. Ili kukomesha ukatili wa ngono katika mizozo juhudi zaidi zahitajika:EU/UN. Matibabu ya kifafa bado ni shida kubwa kwa nchi za kipato cha chini- WHO.  Nzige na Parara ndio chakula cha siku zijazo- Chef Ali

© UNICEF/Pirozzi

Wilaya za Kisarawe na Kibaha nchini Tanzania ni mfano dhahiri wa ujumuishi wa watoto wenye ulemavu- ADD International

Mkutano wa 12 wa nchi wanachama wa mkataba wa watu wenye ulemavu, CRPD ukiingia siku ya pili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, wilaya za Kisarawe na Kibaha mkoani Pwani nchini Tanzania zimetajwa kuwa mfano wa mafanikio ya sera za ujumuishi wa watu wenye ulemavu katika nyanja ya elimu. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

Jimmy Innes, Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la kiraia, ADD linalosaidia kujenga uwezo wa mashirika ya watu wenye ulemavu, ametaja mafanikio hayo akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mkutano huo.

Sauti
1'57"
Jimmy Innes, Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la ADD International linalosaidia mashirika yanayotetea haki za watu wenye ulemavu, akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya UN kando mwa mkutano wa nchi wanachama wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu, CRPD. (11 J
UN News/Assumpta Massoi

Wilaya za Kisarawe na Kibaha zimeitikia wito wa ujumuishi wa watu wenye  ulemavu- ADD International

Mkutano wa 12 wa nchi wanachama wa mkataba wa watu wenye ulemavu, CRPD ukiingia siku ya pili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, wilaya za Kisarawe na Kibaha mkoani Pwani nchini Tanzania zimetajwa kuwa mfano wa mafanikio ya sera za ujumuishi wa watu wenye ulemavu katika nyanja ya elimu.

Sauti
1'57"