Kila nchi lazima ifanye kila iwezalo kujiandaa dhidi ya COVID19:UN
Umoja wa Mataifa umeitaka kila nchi kote duniani kufanya kila liwezekanalo ili kujiandaa endapo mlipuko wa virusi vya Corona COVID19 utazuka.
Umoja wa Mataifa umeitaka kila nchi kote duniani kufanya kila liwezekanalo ili kujiandaa endapo mlipuko wa virusi vya Corona COVID19 utazuka.
Wakati idadi ya maambukizi ya virusi vya corona COVID-19 ikiendelea kuongezeka kila uchao, Shirika la afya ulimwenguni, WHO limehimiza jamii ya kimataifa kuwekeza katika suluhu za afya ambazo zinaweza kusaidia katika kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo sasa na wakati huo huo kusaidia katika kujiandaa kwa ajili ya kuwekeza katika jamii kwa siku za usoni. Grace Kaneiya na ripoti kamili.
Wito huo umetolewa siku chache baada ya taarifa za shirika la fedha duniani, IMF ya makadirio yake kuhusu athari za mlipuko wa virusi vya corona kiuchumi.
Shirika la afya ulimwenguni, WHO, limesema hofya yake hivi sasa juu ya kuenea kwa virusi vya Corona, COVID-19 ni kutokuwa na taarifa za wazi kuhusu uhusiano wa kuenea kwa virusi hivyo, kama vile historia ya mtu kusafiri China au kuwa na mawasiliano na mtu aliyethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.
Shirika la afya duniani WHO linaendesha jukwaa la utafiti na ubunifu ili kuchukua hatua za kimataifa kushughulikia ,mlipuko wa virusi vya corona yaani COVID-2019 ambapo hadi sasa watu 42,000 wameambukizwa na tayari vifo vimefikia zaidi ya 1000.