Coronavirus

 Janga la COVID-19 halijamalizika , muwe makini katika matumizi yenu:IMF

Shirika la fedha duniani IMF limeziasa nchi na watu wote kuwa makini katika matumizi yao kwani athari za kiuchumi zilizosababishwa na janga la corona au COVID-19 hazijaisha na zitaendelea kwa muda.

Mipango kabambe ya kufanikisha watoto kwenda shuleni Kenya

Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa kushirikiana na serikali ya Japan, limechukua hatua kuhakikisha wanafunz

Sauti -
2'27"

Wanahabari wanapolengwa, jamii kwa ujumla ndiyo inalipia gharama-Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia Ujumbe wake alioutoa hii leo mjini New York Marekani kuhusu siku  ya leo ya kimataifa ya kutokomeza ukwepaji wa sheria ya uhalifu dhidi ya wanahabari, amesema katika siku ya mwaka huu, dunia vikiwemo vyombo vya habari, juu ya changamoto nyingine, vimekabiliwa na changamoto mpya kabisa ambayo ni COVID-19. 

30 Oktoba 2020

Katika kuelekea siku ya miji duniani hapo kesho Oktoba 31, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Abtonio Guterres kupitia ujumbe maalum wa siku hiyo amesema miji imebeba gharama kubwa ya janga la corona au

Sauti -
10'48"

WFP na serikali ya Kenya wazindua mpango usaidizi wa kifedha kwa familia zilizoathiriwa na COVID-19 Mombasa, Kenya

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP kwa kushirikiana na serikali ya Kenya leo wamezindua mpango wa ugawaji fedha taslim kwa familia 24,000 mjini Mombasa, Kenya katika makazi yasiyo rasmi ambao maisha yao yamesambaratishwa na athari za janga la COVID-19.

Watoto katika nchi maskini wamepoteza miezi minne ya masomo tangu kuanza kwa janga la COVID-19-Ripoti 

Watoto wa shule katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati chini, tayari wamepoteza takribani miezi minne ya masomo tangu kuanza kwa janga la virusi vya corona ikilinganishwa na wiki sita za upotezaji masomo katika nchi zenye kipato cha juu. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa hii leo mjini New York na Washington Marekani pamoja na Paris Ufaransa na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO na la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na  Benki ya Dunia. 

COVID-19 imetufunza mengi na hata ambayo hatukutarajia: Barubaru Termeh na Toranj 

Kutana na mapacha wawili barubaru kutoka nchini Iran, wanasema janga la corona au COVID-19 limewafunza mengi, kuanzia kusomea nyumbani, kukabiliana na upweke na msongo wa mawazo na hata kupika na  majukumu mengine ya nyumbani. 

COVID-19 imeangusha kwa asilimia 49 aina zote za uwekezaji wa nje wa nchi zilizoendelea.

Mtiririko wa uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni kimataifa, FDI, umepungua kwa asilimia 49 katika nusu ya kwanza ya 2020 ikilinganishwa na mwaka 2019, kwa sababu ya kuanguka kwa uchumi kutokana na COVID-19, umebaini utafiti wa hivi karibuni wa  Monitor mwelekeo wa uwekezaji uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD na kutolewa leo tarehe 27 Oktoba 2020. 

Loise Wairimu-Virusi vya corona vilibadilisha matarajio yangu katika UN lakini nimejifunza SDGs

Janga la ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona limevuruga ndoto za mamilioni ya watu kote duniani.

Sauti -
2'10"

Virusi vya corona vilibadilisha matarajio yangu katika UN lakini nimejifunza SDGs-Loise Wairimu

Janga la ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona limevuruga ndoto za mamilioni ya watu kote duniani. Elimu, afya, biashara, utalii, ukuaji wa kiuchumi na kadhalika vimeyumba kwa kiasi kikubwa.