Filippo Grand aiomba jamii ya kimataifa kutowasahau wakimbizi wa Venezuela.
Maelfu ya wakimbizi wa Venezuela wanavuka mpaka na kuingia Colombia kila siku, wengi wao wakisaka usalama kwa kuhofia maisha yao. Kamishina Mkuu wa wakimbizi Filippo Grandi akihitimisha ziara yake nchini Colombia ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza msaada kwa wakimbizi hawa