12 Aprili 2021
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, kwa kushirikiana na mamlaka nchini Colombia wanatumia kila njia ikiwemo ya kutembea nyumba kwa nyumba ili kuwafikia watu wa jamii za asili walio katika mazingira magumu katika eneo la Amazon kusini mwa nchi ambao ni miongoni mwa makundi ya kipaumbele ya kupatiwa chanjo ya COVID-19.