colombia

Akiwa Colombia, Guterres ajionea maendeleo na changamoto za mkataba wa amani 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko ziarani nchini Colombia, amejionea maendeleo na changamoto za mkataba wa amani uliofikiwa nchini humo miaka mitano iliyopita kati ya serikali na wapiganaji wa zamani wa kikundi cha FARC.

COLOMBIA: UN yalaani mauaji ya waandamanaji mjini Cali

Natoa wito wa kukomeshwa kwa aina yeyote ya vurugu, pamoja na uharibifu, na pande zote kuendeleza mazungumzo, na kuhakikisha maisha ya watu na utu unaheshimiwa na watu wote" Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet

Wakimbizi Wazee nao wanahitaji ajira ili kuweza kujikimu 

Ili kuweza kuishi maisha ya kistaarabu na staha niwajibu kuwa na shughuli ya kukuingizia kipato. Mzee Agapito Andrade mkimbizi raia wa Colombia anayeishi nchini Equador imekuwa ngumu kupata ajira na hivyo hata mlo kwake umekuwa tabu huku janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 likiongeza ugumu maradufukupata ajira.

Vurugu zikiendelea Colombia, Umoja wa Mataifa wataka utulivu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR leo imetoa tahadhari kubwa juu ya vurugu zilizotokea usiku wa kuamkia leo katika mji wa Cali nchini Colombia, ambapo watu kadhaa wameripotiwa kuuawa na kujeruhiwa wakati polisi walipowafyatulia risasi waandamanaji. 

WHO yapita nyumba kwa nyumba ili kuwapatia chanjo ya COVID-19 wanaoishi vijiji vya ndani Colombia

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, kwa kushirikiana na mamlaka nchini Colombia wanatumia kila njia ikiwemo ya kutembea nyumba kwa nyumba ili kuwafikia watu wa jamii za asili walio katika mazingira magumu katika eneo la Amazon kusini mwa nchi ambao ni miongoni mwa makundi ya kipaumbele ya kupatiwa chanjo ya COVID-19.

12 Aprili 2021

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, kwa kushirikiana na mamlaka nchini Colombia wanatumia kila njia ikiwemo ya kutembea nyumba kwa nyumba ili kuwafikia

Sauti -
10'59"

Kamishna Mkuu wa UNHCR aisihi jumuiya ya kimataifa kuiunga mkono Colombia kuwasaidia wavenezuela

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi akiwa ziarani Colombia amesema ukarimu wa Colombia katika kukaribisha wakimbizi wa Venezuela haupaswi kuchukuliwa kwa urahisi na akaomba msaada wa kimataifa kuunga mkono juhudi za nchi hiyo ambazo zinaendelea kulinda watu waliokimbia makazi yao licha ya changamoto za janga la COVID-19.