Tuepushe mlolongo wa chuki unaoweza kusababisha maangamizi ya binadamu- UN
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya waathitrika wa mauaji ya maangamizi makubwa au Holocaust Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema mauaji hayo yalikuwa ni malimbikizo ya miongo ya chuki dhidi ya wayahudi ndio maana sasa ni wakati wa kuhakikisha chuki za aina yoyote ile zinakomeshwa duniani.