Chuja:

Chanjo ya COVID-19

Mwanamke akichomwa chanjo ya pili ya dozi ya COVID19 katika kituo cha afya huko Obassin , Burkina Faso
© UNICEF/Frank Dejongh

Wagonjwa wa COVID19 na Monkeypox waongezeka duniani

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limehimiza nchi wanachama kuhakikisha zinaendelea  kujikinga na janga la COVID19 kwakuwa janga hilo lingalipo na takwimu za wiki mbili zilizopita zinaonesha kuongezeka kwa wagonjwa kwa takriban asilimia 30.

John Kibego

Uganda yaimarisha upatikanaji wa chajo ya COVID-19

Kutokana na vikundi vilivyopewa kipaumbele kwa ajili ya chanjo dhidi ya COVID-19, serikali ya Uganda imeanza kutumia mbinu ya kuchanja mtu mzima yeyote aliyetayari popote pale.

Kwenye maeneo makuu ya ibaada, kwneye hafla na vilevile mitaani watoa chanjo wako tayari kutoa huduma hiyo endapo wanaalikwa na waliotayari.                                                                                                                                          Je, kampeni inatekelezwaje? 
 

Sauti
3'19"

24 Novemba 2021

karibu kusikiliza jarida hii leo Flora Nducha anakuletea mada kwa kina maalum ikiwa ni kelele cha wiki ya kukuza uelewa kuhusu viuajiumbemaradhi, utasikia ushiriki wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula. 

Kabla ya mada hiyo kwa kina utasikia habari kwa ufupi zikiangazia masuala ya COVID-19 ambapo taarifa zinaonesha maambukizi yameendelea kuongezeka hususan barani ulaya lakini barani Afrika yamepungua. 

Pia utasikia kuhusu chanjo ya COVID-19 kwa watoto na Barubaru pamoja na wito uliotolewa kwa nchi zote duniani kuhusu usawa wa kijinsia. 

Karibu. 

Sauti
12'33"
© UNICEF Bhutan/Tshering

Bhutan imefanikiwaje kutoa chanjo kwa asilimia 90 kwa wananchi wake?

Kiwango cha utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19 nchini Bhutan huko barani Asia kimefikia asilimia 90 ya wananchi wote wenye umri wa kupatia chanjo hiyo. Kampeni ya utoaji chanjo imefanywa na serikali ya Bhutan kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.  
 
(Taarifa ya Leah Mushi) 
 
Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF inaanza kwa taswira ya Bhutan, nchi iliyozungukwa na milima ya himalaya ikiwa na eneo lisilozidi kilometa elfu 40 na imepakana na India na China. 
 

Sauti
2'9"