Mkurugenzi mkuu wa Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO José Graziano da Silva katika hotuba yake ya ufunguzi mkutano wa baraza tendaji la shirika huo ulioanza hii leo mjini Roma Italia, amesisitiza kuwa kwa miaka miwili ijayo FAO itajikita katika kukuza mifumo ya chakula cha lishe na uvumbuzi katika kilimo.