Mpango jumla wa hatua za kibinadamu nchini Syria unahitaji karibu dola bilioni 3.3 na kwa sasa umefadhiliwa kwa asilimia 52 kwa jumla, kwa mujibu wa msemaji wa OCHA Jens Laerke.
Baada ya kughubikwa na vita kwa zaidi ya miongo mitatu sasa, ukame wa hivi karibuni umezidisha adha kwa mamilioni ya Wasomali ambao sasa wanahitaji huduma za msingi kama maji, malazi, huduma za afya na chakula.
Ikiwa leo ni siku ya chakula duniani wito ukiwa ni kutokomeza njaa- na kuwa na dunia ambako chakula chenye lishe bora kinapatikana kwa bei nafuu na kwa watu wote na kila mahali, Umoja wa Mataifa unahoji iweje leo hii zaidi ya watu milioni 820 hawana chakula cha kutosheleza mahitaji yao.

Takwimu mpya kufuatia shughuli ya mgao wa chakula mwezi Agosti zinaonyesha kuwa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, lilifikia rekodi mpya kufikishia chakula watu milioni 12.4, wanaokumbwa na uhaba wa chakula mwezi Agosti.
Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema takribani mataifa 41 yanaendelea kuhitaji msaada wa chakula kutoka nje, sababu kuu ikiwa ni mizozo na hali mbaya ya hewa.