Chuja:

CHAKITA

UN News Kiswahili

Neno la wiki-Baba alimpiga binti yake kwa kuwa alilewa

Na leo katika neno la wiki inaelezewa sentensi ambayo imejadiliwa sana kwenye mitandao ya kijamii na kwingine isemayo, baba alimpiga binti yake kwa kuwa alilewa.

Mchambuzi wetu Ken Walibora, mwanariwaya na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA anaelezea sentensi baba alimpiga binti yake kwa kuwa alilewa.

Sauti
58"
UN News Kiswahili

NENO LA WIKI: Kijiko cha jikoni, hakiogopi moto

Neno la wiki limejikita katika kuichambua methali isema, 'Kijiko cha jikoni, hakiogopi moto'.  Mwanariwaya na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA Ken Walibora anasema methali hii kimsingi inaeleza dhana ya kuwa ikiwa mtu ana mazoea fulani au kazoea mazingira fulani, hayamtishi, atatekeleza analolitekeleza bila kuogopa.

Sauti
32"

Utamu wa lugha ni pale inapotumiwa kwa ufasaha.

Kiswahili kimekuwa na mchango mkubwa kwa wazungumzaji wake hususan Afrika Mashariki kikipigwa jeki na vyombo vya habari kama Radio kwa miaka mingi. Lakini sasa hali ikoje katika kukuza na kuendeleza lugha hii?  Ken Walibora ni mwana riwaya na pia amekuwa mwandishi habari akitumia lugha ya Kiswahili miaka nena miaka rudi,  Katika mahojiano ,maalum na Siraj Kalyango wa Idhaa hii amezungumzia lugha hiyo na jinsi vyombo vya habari vinavyohusika kuiendeleza.

Sauti
3'19"
UN News Kiswahili

Neno la wiki - Bumbuwazi

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia neno "Bumbuwazi". Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA . 

Bwana Nuhu anasema unapopigwa na butwaa ama kupatwa na mshangao, hadi ukawa huwezi kuongea hata neno moja basi utakuwa umepigwa na bumbuwazi.

Sauti
13"

Neno la Wiki- Mhanga, Manusura na Muathirika

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno “Mhanga”, "Manusura" na “Muathirika”.  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Ungana naye upate matumizi sahihi ya maneno hayo..

Sauti
58"

Neno la wiki: Mhanga, Manusura na Muathirika

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno "Mhanga", “Manusura” na "Muathirika".  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Ungana naye upate matumizi sahihi ya maneno hayo..