chad

Sitisho la uchimbaji madini Chad laleta zahma kwa wahamiaji

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM linaomba jamii ya kimataifa  dola zaidi ya 500,000 ili kutoa msaada  wa kibinadamu kuweza kurejesha nyumbani maelfu ya wahamiaji walioathiriwa na hatua ya serikali ya Chad, ya  kusitisha shughuli zote za uchimbaji huko Miski na Kouri Bougri, ambayo ni miongoni

Sauti -
1'24"

IOM yaomba msaada kwa wahamiaji waliotimuliwa katika migodi ya dhahabu, Chad

Shirika  la Uhamiaji la  Umoja wa Mataifa,  IOM linaomba jamii ya kimataifa liipatie dola zaidi ya 500,000 ili kutoa msaada wa kibinadamu au kurejesha nyumbani maelfu ya wahamiaji walioathiriwa na hatua ya serikali ya Chad, ya  kusitisha shughuli zote za uchimbaji huko Miski na Kouri Bougri, ambayo ni miongoni mwa machimbo makubwa zaidi ya dhahabu nchini  humo.

Wahusika wa mauaji ya raia huko Borno wasakwe na washtakiwe- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mauaji ya raia wakati wa ghasia zilizotokea huko jimbo la Borno, Kaskazini-mashariki mwa Nigeria.

Mume wangu alinilaghai nijiunge na Boko Haram- Halima

Msichana mmoja nchini Chad ambaye alinusurika kuuwa na bomu alililobebeshwa na Boko Haram ili kufanya mauaji, ameamua kuwa mtoaji wa msaada wa sheria kwa  kwenye ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu,

Sauti -
1'50"

Manusura wa kujilipua ageuka mtoa msaada wa sheria kwa wasichana

Msichana mmoja nchini Chad ambaye alinusurika kuuwa na bomu alililobebeshwa na Boko Haram ili kufanya mauaji, ameamua kuwa mtoaji wa msaada wa sheria kwa  kwenye ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA huko Bol nchini Chad. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Sahel sio ukanda wa zahma bali wa fursa: Thiaw

Ukanda wa Sahel barani ASfrika haupaswi kuchukuliwa kama ukanda wa zahma, badala yake unapaswa kuonekana kama wa fursa, kwa mujibu wa mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Sahel, Ibrahim Thiaw.

Heko Burkina Faso na Benin kwa kufuta adhabu ya kifo- UNOWA

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa nchi za Afrika Magharibi, Mohammed Ibn Chambas amesema licha ya harakati za kidemokrasia kuendelea kushamiri kwenye ukanda huo lbado vikundi vya kigaidi vimeendelea kuwa tishio kwenye ukanda wa Sahel na bonde la ziwa Chad.

Mabadiliko ya tabianchi ni kichocheo tosha cha mizozo-UN

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao kuangazia masuala ya tabianchia na athari zake kwa usalama ambapo Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo amesema, “ni lazima tuelewe mabadiliko ya tabianchi kama suala moja katika mkusanyiko wa vichocheo ambavyo vinaweza kusababisha mzozo” akiongeza kuwa huongeza mzigo juu ya hali dhaifu ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Muda wa maneno umekwisha tuchukue hatua tuokoe wanawake- Bi. Mohammed

Baada ya ziara yao kwenye nchi za Sudan Kusini, Chad na Niger, viongozi wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden, leo wamewasilisha ripoti zao mbele ya wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati wa kikao kuhusu wanawake, amani na usalama barani humo.

Kutana na wavuvi wanawake nchini Chad

Changamoto za mabadiliko ya tabianchi na udhibiti mbaya wa maji , vinawaweka roho juu wanawake wavuvi nchini Chad ambao mlo na maisha yao ya kila siku hutegemea uvuvi, sasa samaki wameanza kuadimika na kuwaongezea mtihani wa kiuchumi na kijamii. Flora Nducha na taarifa kamili

 

Sauti -
2'12"