chad

Sahel sio ukanda wa zahma bali wa fursa: Thiaw

Ukanda wa Sahel barani ASfrika haupaswi kuchukuliwa kama ukanda wa zahma, badala yake unapaswa kuonekana kama wa fursa, kwa mujibu wa mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Sahel, Ibrahim Thiaw.

Uvuvi ndio uhai wetu na maisha yetu , lakini sasa ni mtihani-Wanawake Chad

Navua samaki kwa miaka ishirini,  na sasa inazidi kuwa vigumu kupata samaki, ni kauli ya mvuvi mwanamke huko nchini Chad ambaye mabadiliko ya tabianchi na matumizi holela ya maji kwenye bonde la Ziwa Chad yameleta shida kwenye familia yake

Ziarani Chad, Naibu Katibu Mkuu apazia nafasi ya wanawake

Naibu Katibu Mkuu  wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed yuko ziarani nchini Chad ambako amesisitiza jukumu muhimu la wanawake wa nchi hiyo katika kukabiliana na changamoto za Boko Haram na uchochezi wa ukatili.

Usalama waimarika Darfur, waliokimbia waanza kurejea

Kuimarika kwa hali ya usalama jimboni Darfur nchini Sudan kumesababisha awamu ya kwanza ya wakimbizi waliosaka hifadhi nchini Chad kurejea jimboni humo wiki hii.

Misaada ya kujikwamua ni muhimu zaidi kwa wakimbizi Chad

Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na  usaidizi wa majanga, OCHA, Ursula Mueller amehitimisha ziara yake huko Chad iliyolenga kujionea hali halisi ya athari za mashambulizi yanayofanywa na Boko Haram. 

UNHCR yasaka dola milioni 157 kusaidia wahanga wa Boko Haram

The United Nations High Commissioner for Refugees (UNHCR), along with its humanitarian partners, today launched a $ 157 million fundraising drive to help more than a quarter of a million people affected by Boko Haram attacks in the basin. lake Chad.