Kamati ya UN yakubaliana na uamuzi wa FIFA dhidi ya Rais wa Soka Hispania
Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kutokomeza Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW) imekaribisha uamuzi wa kusimamishwa kazi kwa mkuu wa soka wa Uhispania Luis Rubiales, hatua iliyochukuliwa na FIFA baada ya kumbusu kwa lazima nahodha wa soka wa Uhispania Jennifer Hermosa wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo ya Kombe la Dunia la Wanawake mwaka 2023 (WWC23).