Ugonjwa wa fistula unatibika. Mimi ni shuhuda - Magreth Rubeni
Leo tarehe 23 Mei 2022 ni Siku ya Kutokomeza Ugonjwa wa Fistula kauli mbiu yam waka huu ikiwa ni “Tokomeza Fistula, wekeza, imarisha ubora wa huduma za afya na wezesha jamii”. Ugonjwa wa Fistula ya uzazi huwapata wanawake wakati wa kujifungua hasa wale wanaojifungua wakiwa na umri mdogo pamoja na kukosa msaada stahiki wakati wa kujifungua, ambapo viungo kama kibovu cha mkojo na njia ya haja kubwa hujeruhiwa na kusababisha mwanamke ashindwe kujizuia haja ndogo au kubwa. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani (WHO).