Tatizo la wanawake kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua linaonekana kupata tiba mujarabu baada ya wataalamu kubaini dawa mpya isiyohitaji kuhifadhiwa kwenye jokofu kama ilivyo kwa dawa ya sasa iitwayo Oxytocin.
Katika nchi zinazoendelea, vifo vya wanawake vitokanavyo na kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua linaendelea kuwa mwiba kutokana na changamoto ya uhifadhi wa dawa ya kuzuia tatizo hilo.