BIASHARA YA UJI

06-12-2018

Umoja wa Mataifa umetaja mambo matatu ambayo unatamani yatokane na mkutano zinazokinzana nchini Yemen. Muhitimu wa chuo kikuu nchini Tanzania baada ya yeye mwenyewe kukosa ajira, sasa ageuka kuwa mwajiri kupitia biashara ya uji.

Sauti -
12'19"

Elimu si karatasi, ni kuelimika

Makadirio ya shirika la kazi duniani ILO yaliyotolewa mwaka uliopita wa 2017, yalionesha kuwa upatikanaji wa ajira kwa vijana utaendelea kuzorota kwa  mwaka huu wa 2018 ambapo vijana milioni 71.1 sawa na asilimia 13.1 ya vijana wote kote duniani hawatakuwa na ajira. Miongoni mwa vijana hao wasiokuwa na fursa ya kupata ajira rasmi ni Situmai Simba msichana mwenye umri wa miaka 24 aliyeanzisha biashara ya uji, ambao kutokana na ubunifu, anamudu kupambana na hali hii ya ukosefu wa ajira kwa kubuni miradi mipya inayowaajiri wao na wenzao.