Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Bentiu

15 AGOSTI 2022

Hii leo jaridani tunamulika mwaka mmoja wa watalibani madarakani nchini Afghanistani na madhara yake kwa watoto wa kike. “Watoto wa kike hawaruhusiwi kuendelea na masoko ya elimu ya sekondari.”
Kisha Sudan Kusini ambako walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanahaha kuondoa maji ya mafuriko yaliyotwama kwenye mji wa Bentiu, jimboni Unity.
Makala tunaye kijana Gloria Anderson Mkurugenzi wa shirika la TEDI Tanzania ambalo linahamasisha elimu inayoendana na hali ya sasa ya sayansi na teknolojia ili kuwaandaa wanafunzi kuanzia ngazi za chini kuweza baadaye kujiajiri na kuajiriwa.

Sauti
12'34"