Benki ya Dunia

Benki ya Dunia yaondoa adha ya jenereta kwa wakazi wa Goree, Senegal

Mradi wa Benki ya Dunia wa kutandaza nyaya za umeme baharini, umeondoa adha ya kukatika umeme mara kwa mara iliyokuwa ikikumba wakazi wa kisiwa cha Gorée nchini Senegal. 

Gharama ya juu ya nyumba EU yakatisha tamaa vijana- Ripoti

Hatma ya mamilioni ya vijana kupata ajira kwenye miji mikuu ya Muungano wa Ulaya, EU iko mashakani kutokana na bei za nyumba kuwa ni za juu kupita kiasi sambamba na kodi ya pango.

Mazingira bora ya biashara Afghanistan yaleta matumaini

Mkakati wa serikali ya Afghanistan wa kupunguza umaskini, kufungua fursa za ajira na kuboresha mazingira ya biashara umeanza kuzaa matunda na kuimarisha sekta binafsi nchini humo. 

Ripoti ya Benki ya Dunia yasema uchumi wa Kenya na rwanda umebaki thabiti.

Kasi ya  ukuaji uchumi kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ni ndogo kuliko ilivyotarajiwa, imesema ripoti mpya ya Benki ya Dunia kwa mwezi huu wa Oktoba. 

Sauti -
1'47"

Rwanda, Kenya na Côte d’Ivoire kidedea ripoti ya Benki ya Dunia

Kasi ya  ukuaji uchumi kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ni ndogo kuliko ilivyotarajiwa, imesema ripoti mpya ya Benki ya Dunia kwa mwezi huu wa Oktoba. Siraj Kalyango na ripoti kamili.

Kutoka ufukara hadi kujenga uzio wa shamba, asante Benki ya Dunia

Mradi wa Benki ya Dunia na serikali ya Afghanistan wa kuhamasisha wanakijiji kujitegemea kupitia biashara ndogo umewezesha jamii kujikwamua kiuchumi na kijamii.

Twashona nguo, twafuga, umaskini kwaheri- Wanufaika wa mradi wa Benki ya Dunia Afghanistan

Mradi wa Benki ya Dunia na serikali ya Afghanistan wa kuhamasisha wanakijiji kujitegemea kupitia biashara ndogo umewezesha jamii kujikwamua kiuchumi na kijamii.

Sauti -
1'41"

Benki ya Dunia yaishika mkono Bangladesh ili iboreshe huduma kwa warohingya

Benki ya Dunia imechukua hatua kusaidia Bangladesh kuimarisha huduma za afya  ili nchi hiyo iweze kukabiliana na mahitaji ya wakimbizi wa Rohingya waliosaka hifadhi eneo la Cox’s Baz ar nchini humo.

Katika kila sekunde 5 mtoto 1 alifariki dunia mwaka 2017 kwa magonjwa yanayozuilika- UNICEF

Takribani watoto milioni 6.3 wenye umri wa chini ya miaka 15 walifariki dunia mwaka jana kutokana na magonjwa yanayozuilika, imesema ripoti mpya iliyotolewa na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Teknolojia yaweza kuwa mkombozi wa maendeleo duniani:FOSS4G 2018

Mkutano wa kimataifa wa kutumia ubunifu wa ramani mtandaoni kufuatia picha zilizopigwa na ndege zisizokuwa na rubani au drones, unaendelea hivi sasa jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, ukiwaleta pamoja wadau zaidi ya1000 kutoka nchi mbalimbali duniani.