Baraza la usalama

Suluhu ya zahma ya Rohingya lazima itoke Myanmar: UN

Suluhu ya zahma ya Rohingya inayoendelea ni lazima itoke nchini Myanmar, umesema leo Umoja wa Mataifa.

Dunia tuliyonayo ni moja tu hakuna haja ya kuiharibu-Guterres

Sisi binadamu hatuna rukhsa  ya kuangamiza hii dunia moja tuliyo nayo, ama kukubali tofauti zetu kusababisa mateso na maumivu ambayo yanatuzuia kufaidika na manufaa ya ustaarabu.

UN yaiasa jamii kutofumbia macho suala la ukatili dhidi ya wanawake mashinani

Ukatili wa kingono katika maeneo ya vita na machafuko umebainika kuwa moja ya sababu kubwa za watu kutawanywa.

Sauti -
2'28"

Ubabe wa wajumbe Barazani kuendelea kutesa wasyria

Vuta ni kuvute baina ya wajumbe wa Baraza la Usalama kuhusu sakata la madai ya matumizi ya silaha za kemikali huko Douma nchini Syria, imeendelea hii leo baada ya maazimio mawili tofauti yaliyowasilishwa mbele yao mchana wa leo Jumanne kugonga mwamba.

Sauti -
2'16"

Urusi yasema katu isihusishwe na kilichotokea Douma

Kufuatia madai ya matumizi ya silaha za kemikali huko Douma nchini Syria, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili suala hilo ambapo Umoja wa Mataifa unaelezea masikitiko yake huku Urusi ikikanusha kuhusika kwa njia yoyote ile.

Burundi, twaheshimu mamlaka yenu lakini mwatutia wasiwasi

“Ni muhimu pande zote hususan serikali itangaze ahadi yake kwenye mchakato unaoongozwa na Jumuiya Afrika Mashariki, na kufikia makubaliano kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2020”

Damu iliyomwagika leo Gaza inatosha

Naibu msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kisiasa Tay Brook Zerhoun ametoa wito kwa vikosi vya usalama vya Israel kujizuia ili kuepuka zahma zaidi kwa raia wa Gaza, akisisitiza kuwa matumizi ya nguvu iwe ni suluhu ya  mwisho, na kutaka uchunguzi wa kina ufanyike dhidi ya mauaji yaliyotokea.

Baraza la Usalama: mapigano kukoma kwa siku 30 Syria

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio namba 2401 la usitishwaji wa mapigano kwa siku 30 katika eneo la Ghouta mashariki nchini Syria na mji mkuu Damascas, ili kupisha  misaada ya kibinadamu.

Katiba ya UN iende na wakati ili kukidhi mahitaji- Guterres

Kupatia suluhu changamoto kama vile athari za mabadiliko ya tabianchi, uhamiaji na ukosefu wa usawa ni majaribio makubwa sana kwa Katiba ya Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha dunia inakuwa bora kwa watu wote.