Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana Jumatano kenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, kujadili hali ya Nicaragua kwa ombi maalumu la Marekani licha ya upinzani wa kufanya hivyo kutoka kwa Urusi, China, Bolivia na Ethiopia, ambao hawadhani hali nchini Nicaragua ni tishio la amani ya kimataifa.