Baraza la usalama

Suluhu ya zahma ya Rohingya lazima itoke Myanmar: UN

Suluhu ya zahma ya Rohingya inayoendelea ni lazima itoke nchini Myanmar, umesema leo Umoja wa Mataifa.

Urusi yasema katu isihusishwe na kilichotokea Douma

Kufuatia madai ya matumizi ya silaha za kemikali huko Douma nchini Syria, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili suala hilo ambapo Umoja wa Mataifa unaelezea masikitiko yake huku Urusi ikikanusha kuhusika kwa njia yoyote ile.

Burundi, twaheshimu mamlaka yenu lakini mwatutia wasiwasi

“Ni muhimu pande zote hususan serikali itangaze ahadi yake kwenye mchakato unaoongozwa na Jumuiya Afrika Mashariki, na kufikia makubaliano kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2020”

Baraza la Usalama: mapigano kukoma kwa siku 30 Syria

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio namba 2401 la usitishwaji wa mapigano kwa siku 30 katika eneo la Ghouta mashariki nchini Syria na mji mkuu Damascas, ili kupisha  misaada ya kibinadamu.

Vita dhidi ya ISIL vyaingia awamu mpya:Voronkov

Hii leo kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wajumbe wameelezwa kuwa ingawa yaonekana kuwa magaidi wa ISIL wamesambaratishwa baadhi ya maeneo, bado kundi hilo ni tishio kwa kuwa limeibuka na mbinu mpya za kusajili wafuasi wanaoweza kufanya mashambulizi ya hapa na pale.