Baraza Kuu -GA na Baraza la Usalama

Timu ya dharura ya IOM yawasili Nepal kutoa msaada

Wafayankazi wa dharura wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM wamewasili nchini Nepal kuisaidia serikali na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu kukabiliana na athari za tetemeko la aridhi la tarehe 25 ambalo limesababisha madhara makubwa na kupoteza maisha ya watu wengi.

Sauti -

Wavulana 282 na msichana mmoja waachiliwa na kundi la Sudan Kusini

Wavulana 282 na msichana mmoja waachiliwa na kundi la Sudan Kusini

Wavulana 282 na msichana mmoja wameachiliwa huru katika hatua ya mwisho ya kuwaachilia watoto waliokuwa wanahusishwa na kushikiliwa na kundi la watu wenye silaha la Cobra Sudan Kusini.

Sauti -

Kuendelea kushikiliwa mahabusu waandishi habari wa Ethiopia hakukubaliki:UM

Kuendelea kushikiliwa mahabusu waandishi habari wa Ethiopia hakukubaliki:UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa maoni na kujieleza David Kaye,na mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu uhuru wa uwanachama na kukutana kwa amani Maina Kiai, leo wamesema kushikiliwa mahabusu kwa wanablogu sita wajulikanao kama “Zone Nine” na waandishi habari wengine

Sauti -

Suala la kushambulia meli zilizobeba wahamiaji halina mashiko:Kutesa

Suala la kushambulia meli zilizobeba wahamiaji halina mashiko:Kutesa

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Sam Kutesa amepinga wazo la nchi za Muungano wa Ulaya la kutaka kushambulia kwa bomu meli zote zitakazokuwa zinavuka bahari ya Mediteranea zikiwa na wahamiaji na wakimbizi wanaokwenda kusaka  hifadhi barani humo.

Sauti -

Hatua zaidi zatakiwa wasichana wajiunge na TEKNOHAMA: ITU

Hatua zaidi zatakiwa wasichana wajiunge na TEKNOHAMA: ITU

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wasichana katika masuala ya ya habari, mawasiliano na teknolojia, TEKNOHAMA, shirika la Umoja wa Mataifa la mawasiliano, ITU limetaka kubadilika kwa mtazamo kuhusu wasichana kujiunga na sekta hiyo ili idadi yao iweze kuongezeka.

Sauti -