Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu, CAR, kwa kushirikiana na wadau wameanzisha mradi wa kuwajengea uwezo wapiganaji waliosalimisha silaha zao na kuwa raia wema.
Huko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu, MINUSCA unaendesha mafunzo yenye lengo la kupunguza ghasia na kuleta maelewano baina ya jamii, CVR.
Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR amelaani vikali shambulio dhidi ya hospitali nchini humo na kusema sio ubinadamu na haustahili na ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu.
Awali wananchi walipata shida kufika polisi ili kueleza madhila yao, lakini hivi sasa Umoja wa Mataifa umeweka mazingira ambamo kwayo wananchi wanaripoti polisi madhila yanayowakumba kwa urahisi na pia bila gharama yoyote.
Wakimbizi wa Sudan waliokuwa kwenye kambi za Bambari nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, wameanza kurejeshwa kwa hiyari nyumbani kufuatia uzinduzi wa zoezi hilo unaondeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi