Balozi Kenedy Gastorn

UN News/Anold Kayanda

Siku ya Kiswahili Duniani ni zawadi ya Tanzania kwenda duniani: Balozi Gastorn

Kutangazwa kuwa na siku maalum ya kuadhimisha lugha ya Kiswahili duniani ni zawadi kubwa kutoka Tanzania kwenda duniani na hii ni furaha kubwa sana amesema mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Profesa Kennedy Gastorn akielezea hisia zake baada ya wiki iliyopita shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO kupitisha azimio la kuifanya tarehe 7 Julai kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani. 
(CLIP BALOZI KENENDY) 

UN News/Anold Kayanda

Siri ya Tanzania katika kuidhibiti COVID-19

Wakati hii leo, wakuu wa nchi na wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanashiriki mkutano wa ngazi ya juu wa UNGA75 wa kujadili jinsi ya kuepusha upotoshaji wa taarifa na usambazaji wa taarifa potofu wakati huu wa janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19, Tanzania imetaja siri ya mafanikio yake katika kudhibiti gonjwa hilo mara baada ya kubainika mwezi Machi mwaka huu. Flora Nducha na maelezo zaidi. 

Sauti
1'56"