AstraZeneca

Walinda amani Jamhuri ya Afrika ya kati: Ulinzi tulionao kwa wakati huu ni chanjo

Kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR imezinduliwa mwanzoni wa wiki hii kwa kuwa walinda amani ni moja ya makundi ya kipaumbele.  Taarifa ya Anold Kayanda inaeleza zaidi.

Sauti -
1'46"

Ulinzi tulionao kwa wakati huu ni chanjo – Walinda amani Jamhuri ya Afrika ya kati 

Kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR imezinduliwa mwanzoni wa wiki hii kwa kuwa walinda amani ni moja ya makundi ya kipaumbele. 

COVAX yawasilisha dozi zaidi ya 350,00 za chanjo ya COVID-19 Niger

Serikali ya Niger leo imepokea Zaidi ya dozi 350,000 za chanjo dhidi ya corona au COVID-19 kupitia mkakati wa kimataifa wa kuhakikisha kila nchi inapata chanjo unaosimamiwa na Umoja wa Mataifa COVAX.

Zaidi ya nchi 100 zimepokea chanjo dhidi ya Covid-19 kupitia COVAX

Zaidi ya nchi 100 zimepokea chanjo dhidi ya Covid-19 kupitiaCOVAX, ambao ni utaratibu wa mshikamano wa kimataifa uliowekwa na Umoja wa Mataifa na washirika wake kuhakikisha usambazaji wa chanjo kwa uharaka, usawa, salama na ubora. 

Uhusiano kati ya kuvia damu na chanjo ya AstraZeneca wawezekana lakini haujathibitishwa- WHO

Kamati ndogo ya kamati ya kimataifa ya kushauri shirika la afya la Umoja wa Mataifa ulimwenguni, WHO, kuhusu usalama wa chanjo imesema uhusiano wa binadam kuvia damu baada ya kupatiwa chanjo ya AstraZeneca unawezekana kuwepo lakini bado kuthibitishwa.
 

Chanjo ya Johnson & Johnson ruksa kutumika licha ya hofu ya kuganda kwa damu:WHO

Chanjo ya Janssen  dhidi ya virusi vya COVID-19  leo imeidhinishwa hadharani kwa matumizi ya kimataifa na bodi ya ushauri ya wakala wa afya wa shirika la Umoja wa Mataifa SAGE, ambayo pia imeondoa wasiwasi wa kuganda kwa damu kunakohusishwa na nchi zingine dhidi ya chanjo za COVID-19 , bila kuwa ushahidi dhahiri